Kubusu msahafu unapodondoka kutoka mahali pa juu


Swali: Ni ipi hukumu ya kubusa msahafu wakati unapodondoka kutoka mahali pa juu?

Jibu: Hatujui dalili juu ya uwekwaji Shari´ah wa kuubusu. Lakini hapana neno mtu akiubusu. Kwa sababu imepokelewa kutoka kwa ´Ikrimah bin Abiy Jahl (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye ni Swahabah mtukufu, kwamba alikuwa akiubusu msahafu na akisema:

“Haya ni maneno ya Mola wangu.”

Kwa hali yoyote kubusu hakuna neno. Lakin sio jambo lililowekwa katika Shari´ah na hakuna dalili juu ya uwekwaji Shari´ah wa jambo hilo. Lakini mtu akiubusu hali ya kuwa ni mwenye kuutukuza na kuuheshimu wakati unapodondoka kutoka mikononi mwake au kutoka mahali pa juu hapana neno kufanya hivo – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/289)
  • Imechapishwa: 16/07/2021