Swali: Ni ipi hukumu ya kunyanyua mikono katika du´aa ya Qunuut, kupangusa uso na mikono na kuibusu baada ya kumaliza kuomba du´aa hiyo?

Jibu: Kuhusu kunyanyua mikono katika du´aa ya Qunuut ni sahihi. Imethibiti kutoka kwa ´Umar na baadhi ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) kama Abu Hurayrah.

Kuhusiana na kupangusa uso baada ya kuomba du´aa sio Sunnah, ni mamoja katika Qunuut na sehemu nyinginezo.

Ama kuibusu ni jambo ambalo liko mbali kabisa na Sunnah. Haikuwekwa ya kwamba mtu anapomaliza kuomba du´aa akabusu mikono yake.

Kwa hivyo, kunyanyua mikono ndio Sunnah. Kuhusu kupangusa na kuibusu sio Sunnah. Lakini hata hivyo kuhusu kupangusa ni jambo limekuja katika Hadiyth dhaifu. Ama kuibusu haikuja katika Hadiyth si Swahiyh wala dhaifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 03
  • Imechapishwa: 23/09/2020