Kubisha hodi kwanza kabla ya kuingia chumbani kwa mahram zako


Swali: Ikiwa kwenye nyumba kuna Mahram wangu na mimi siishi pamoja nao, nikiwatembelea niombe kwanza idhini [kabla ya kuingia ndani kwenye chumba alipo] au hapana?

Jibu: Ni lazima kuomba kwanza idhini. Hata kwa mke wako ni lazima kuomba idhini kwanza. Usimwingilie tu moja kwa moja isipokuwa mpaka kwanza ufanye kitu cha kumzindua [kwamba unaingia kule alipo]. Kwa sababu anaweza kuwa katika hali ambayo haridhii umuone.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-11-02.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014