Kubeba mtoto aliyejisaidia katika nebi yake

Swali: Ni ipi hukumu ya kumbeba mtoto katika swalah na ambaye wakati mwingine anakuwa na najisi?

Jibu: Hakuna neno. [Najisi hiyo] inasamehewa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimbeba Umaamah, ambaye alikuwa mjukuu wake, ilihali yuko anaswali pindi alipokuwa bado msichana mdogo. Kunasamehewa kwa hayo na hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 17/04/2017