Kubaki na mfanyikazi wa kike nyumbani


Swali: Naishi na shangazi yangu ambaye ni mwenye mwili wa kupoza. Ana watoto ambao mkubwa katika wao ana miaka nane. Ana mfanyikazi wa kike. Wakati mwingine shangazi yangu hutoka na kwenda kazini na mimi, watoto na huyo mfanyikazi wa kike tunabaki nyumbani. Je, kuna kosa kufanya hivo?

Jibu: Watoto wadogo hawasaidii kitu. Watoto wadogo ambao hawawezi kupambanua mambo hawasaidii kitu. Ikiwa ni wenye uwezo wa kupambanua hakuna neno. Ama wakiwa ni chini ya uwezo wa kupambanua hawasaidii kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017