Kubadili mahali pa kutekelezea Sunnah baada ya swalah

Swali: Je, kumepokelewa juu ya kubadili mahali pa kutekelezea Sunnah baada ya swalah kinachofahamisha juu ya kupendeza kwake?

Jibu: Hakukupokelewa juu ya hilo Hadiyth Swahiyh kutokana na ninavojua. Lakini Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na wengi katika Salaf walikuwa wakifanya hivo. Jambo ni lenye wasaa. Kumepokelewa juu yake Hadiyth dhaifu kwa Ibn Daawuud (Rahimahu Allaah) na linaweza kutiwa nguvu na kitendo cha Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhum) na wale wema waliotangulia waliofanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/378)
  • Imechapishwa: 09/11/2021