Swali: Kuba lilioko juu ya kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni la kikafiri na la haramu?

Jibu: Hapana, sio kuba la kikafiri. Hakuna anayefanya Tabarruk kwalo, hakuna ambaye yuko na imani fulani juu yake, hakufanywi Twawaaf kwalo. Limejengwa kwa sababu tu ya kuipa kivuli na kuilinda kaburi. Lililo bora ni kutokuwepo, lakini aliyelijenga ni mtawala mmoja hivi. Mtawala ndiye aliyelijenga na hakushauriana na wanachuoni. Ni jambo limetoka kwa mtawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (30) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2019%20-%2010-%20-1436.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017