Kuazimia mema na maovu na mtu asiyafanye  

Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

37- Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema kutokana na yale aliyoyapokea kutoka kwa Mola Wake, hali ya kuwa ni Mwenye kutukuka, ya kwamba Amesema:

“… atakayeazimia kufanya tendo jema kisha asiweze kulifanya, basi Allaah atamwandikia ujira wa tendo jema lililokamika.”

Hili linahitajia ufafanuzi:

1- Akiliacha kwa kumuogopa Allaah (Jalla wa ´Alaa) na kutaraji thawabu kutoka Kwake, basi anaandikiwa thawabu moja kama ilivyotajwa katika Hadiyth hii. Akiiacha kwa ajili ya Allaah (Jalla wa ´Alaa), huyu anaandikiwa thawabu moja. Ikhlaasw yake imemzuia na ovu lile na badala yake kwenda katika tendo zuri. Kukusudia na kuazimia kutenda tendo nzuri mtu anaandikiwa kwa hilo jema moja.

2- Mtu aazimie kufanya tendo ovu na asilifanye kwa ajili ya kutokuwa na uwezo na wakati huo huo nafsi bado imebaki hali ya kutamani kulifanya. Huyu hata kama hakufanya tendo hili haandikiwi thawabu kwa ajili ya hilo. Bali kinyume chake akijaribu kuleta sababu za maasi, basi ataandikiwa dhambi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 504
  • Imechapishwa: 10/05/2020