Kuapa kwa talaka si kama kuapa kwa asiyekuwa Allaah

Swali: Ni ipi hukumu kwa yule mwenye kuridhia kuapa kwa Talaka na wala haridhii kuapa kwa Allaah?

Jibu: Kuapa kwa Talaka haina maana kama ya yamini, kuapa kwa asiyekuwa Allaah. Maana yake ingekuwa hii, mwenye kuapa angelikuwa ni mshirikina kama yule anayeapa kwa asiyekuwa Allaah. Imeitwa kuapa kwa kuwa inafanana na kuapa. Kwa kule kutaka kwake kuhimiza jambo, kusadikisha jambo au kulikadhibisha. Kaiegemeza Talaka juu ya kitu akikusudia kukihimiza, kukikataza, kusadikisha au kukadhibisha khabari. Ikawa imefanana na yamini kwa uwajibu wa kutoa kafara na si kwamba ni yamini ya hakika. Na kwa sababu hii ndio maana hazingatiwi kuwa ni mshirikina kama yule anayeapa kwa asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jalla). Kuna tofauti kati ya hili na hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/3242
  • Imechapishwa: 03/03/2018