Kuanzwe swalah ya faradhi au swalah ya kupatwa kwa jua?

Swali: Mtu aanze na kitu gani ikiwa mwezi utapatwa baada ya kuingia wakati wa swalah?

Jibu: Kunatakiwa kuanzwe swalah ya faradhi. Kwa mfano mwezi umepatwa baada ya kuadhiniwa. Katika hali hii tunasema kuanze kuswaliwa swalah ya faradhi kisha ndio kuje swalah ya kupatwa kwa jua. Kwa nini? Mosi ni kwa sababu swalah ya faradhi ndio muhimu zaidi na ni wajibu.

Pili ni kwa sababu swalah ya faradhi ndio yenye kupendwa zaidi na Allaah. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema katika Hadiyth ya kiungu:

“Mja hatojikurubisha kwangu kwa kitu ninachokipenda zaidi kuliko yale niliyomfaradhishia.”

Tatu ni kwa sababu ni jambo jepesi zaidi kwa watu. Kwa sababu watu wakiswali swalah ya faradhi huenda wana mambo ya kufanya, wanahitajia kukidhi haja ndogo, haja kubwa au mengineyo.

Nne iwapo wataanza kuswali swalah ya kupatwa kwa jua na akaja mtu ambaye ameingia baada ya imamu kumaliza kupiga Takbiyr hatojua anuie kitu gani na atanuia kuwa ni swalah ya faradhi ilihali ni swalah ya kupatwa kwa jua. Kwa hiyo ndio maana tunasema kuwa watu waanze kuswali kile ambacho kiko karibu kwenye akili za wale wenye kuingia. Nacho ni swalah ya faradhi.

Kwa kifupisha ni kwamba watu waanze kuswali swalah ya faradhi kabla ya swalah ya kupatwa kwa jua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (72) http://binothaimeen.net/content/1648
  • Imechapishwa: 04/04/2020