Swali:  Kuanzisha kundi linalopingana na mtawala kunazingatiwa ni kufanya uasi na moja katika mfumo wa Khawaarij?

Jibu: Ndio. Huu ndio mfumo wa Khawaarij. Kupingana na mtawala na kuanzisha kundi linalompinga. Hapana shaka kwamba huku ni kufanya ausi. Ni aina moja wapo ya kufanya uasi dhidi ya mtawala.

Lililo wajibu ni kusikiliza na kuwatii watawala wa waislamu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa kweli mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri zaidi.” (04:59)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
  • Imechapishwa: 01/01/2018