Swali: Kuna mradi tulikuwa tumeanzisha “Majallatu lil-Atwfaal-il-Muslimiyn” kwa jina “Arwaa” ambapo tutakutumia nuskha yake. Alikuja mtu ambaye tunamuamini kwa dini yake ambapo akapingana na sisi kwa njia ya kuchora watu pamoja na kujua ya kwamba tulijiepusha kuwachora Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Pamoja na haya yote akatwambia aliyotwambia. Kwa hiyo tunakuomba jawabu isemavyo Shari´ah kuhusu yale tuliyoyafanya.

Jibu: Kuchukua picha viumbe vilivyo na roho ni haramu. Haijalishi kitu hata kama ni picha za wengine wasiokuwa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Kitendo cha kwamba zinaweka wazi zaidi na kupendezesha hakitakasi kuruhusiwa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=141979
  • Imechapishwa: 22/04/2018