Kuanza kwa kusoma Qur-aan katika sherehe mbalimbali


Swali: Ni ipi hukumu ya kuanza kwa maneno ya Allaah katika sherehe mbalimbali?

Jibu: Hakuna neno kule kusoma Kitabu cha Allaah. Lakini watu wote wanatakiwa kuyazingatia, kuyatafakari na kuyafahamu. Ama kusoma peke yake bila kutilia umuhimu na bila kusikiliza na huku watu wamejishughulisha kutokamana nayo na wanazungumza ni jambo lisilotakikana. Kitabu cha Allaah kitukufu Allaah amekiteremsha kwa ajili ya uongofu, kisomwe na kitendewe kazi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/45/%D8%A7%D8%A8%D8%AA%D8%AF%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AD%D8%A7%D9%81%D9%84-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%A7%D8%AC%D8%AA%D9%85%D8%A7%D8%B9%D8%A7%D8%AA-%D8%A8%D9%82%D8%B1%D8%A7%D8%A1%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%B1%D8%A2%D9%86
  • Imechapishwa: 18/01/2020