Swali: Je, inafaa kuandika Basmalah katika kadi za ndoa kwa kuzingatia kwamba baada ya hapo zinatupwa kwenye mabarabara na mapipa ya taka?

Jibu: Ni jambo limesuniwa kuandika Basmalah katika kadi na nyujumbe nyenginezo. Hilo ni kutokana na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amesema:

”Kila jambo lililo na umuhimu lisiloanzwa kwa Jina la Allaah, basi limeondoshewa baraka.”

Isitoshe yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akianza nyujumbe kwa jina la Allaah.

Haijuzu kwa yule atakayepewa kadi iliyoandikwa utajo wa Allaah au Aayah ya Qur-aan akaitupa mahali pa taka, jalala au akaiweka mahali ambapo inayodharauliwa. Vivyo hivyo magazeti na vitu mfano wake. Haijuzu kuvitweza wala kuvitupa mahali pa taka, kuifanya ni meza ya chakula wala faili ya haja kutokana na ule utajo wa Allaah uliyotajwa ndani yake. Dhambi zinakuwa kwa yule aliyefanya kitendo hicho na si yule aliyeandika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/427)
  • Imechapishwa: 07/02/2021