Kuamka na janaba dakika moja kabla ya wakati kumalizika

Swali: Kuna mtu ameamka na janaba wakati wa Rak´ah moja kabla ya wakati wa swalah kutoka. Je, atangulize kujitwaharisha au wakati?

Jibu: Ikiwa yuko na maji atangulize kujitwaharisha. Asiswali na yuko na janaba. Ikiwa anahitaji kutafuta maji kwanza au kununua, afanye Tayammum na kuswali. Ama ikiwa yuko na maji asiswali mpaka ajitwaharishe kwanza hata kama wakati utatoka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/msrf–16041434.mp3
  • Imechapishwa: 24/09/2020