Kuahirishwa kwa Hijjah mwaka 317

Mwaka 317 al-Muqtadir na Mansuur ad-Daylamiy wakaondoka na msafara na wakafika Makkah wakiwa wamesalimika. Tarehe 8 Dhul-Hijjah wakavamiwa na adui wa Allaah Abu Twaahir al-Qarmatwiy. Akawaua mahujaji katika msikiti Mtakatifu, katika njia za Makkah na ndani ya Nyumba. Akamuua Ibn Muhaarib mkuu wa Makkah na akaifanya Nyumba kuwa tupu, akang´oa mlango wake na akalitoa jiwe jeusi ambalo baadaye akalichukua. Akawatupa wale wafu ndani ya Zamzam. Akarejea katika mji wake Hajar akiwa na jiwe lake jeusi kama mali. Njia zote za Makkah zikajaa wauliwaji. Abu Bakr Muhammad bin ´Aliy bin al-Qaasim adh-Dhahabiy amesema katika kitabu chake cha historia:

”Abu Twaahir Sulaymaan Hasan al-Qarmatwiy kutoka Bahrain aliingia Makkah na wanamme 700.  Akaua katika msikiti Mtakatifu karibu watu 170.000 wanamme na wanawake wakiwa wamesimama na kuning´inia katika pazia za Ka´bah. Akajaza Zamzam wafu wake, akapanda juu ya Ka´bah, akawageukia watu akisema:

Mimi ni kupitia Allaah

na kupitia Allaah ndiye mimi

Amewaumba viumbe

wameteketezwa na mimi[1]

Kwenye vichochoro na njia za Makkah waliuliwa watu 30.000 na wanawake na watoto 30.000 wakashikwa mateka. Alibaki Makkah kwa muda wa siku sita. Tarehe 7 Dhul-Hijjah akawashambulia watu. Mwaka huo hakuna yeyote aliyesimama ´Arafah. Allaah akamuadhibu kwa kumpa maradhi mwilini na yakarefuka mpaka yakamkatakata viungo vyake.

[1] Taariykh Akbaar-il-Qaraamitwah (54), al-´Ibar (2/168), Duwal-ul-Islaam (1/192), Miraat-ul-Jinaan (2/272) na al-Bidaayah wan-Nihaayah (11/160).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taariykh-ul-Islaam (23/380)
  • Imechapishwa: 18/04/2020