Swali: Wakati mwingine huswali swalah za faradhi peke yangu kwa sababu ya kutokuweko msikiti karibu yangu. Je, inanilazimu kutoa adhaana na kukimu juu ya kila swalah au inafaa kuswali pasi na adhaana au kukimu?

Jibu: Sunnah ni wewe kutoa adhaana na kukimu. Kusema kwamba ni lazima ni jambo wanazuoni wametofautiana. Lakini bora na lililo salama zaidi kwako ni wewe kuadhini na kukimu kutokana na ueneaji wa dalili. Lakini inakulazimu kuswali katika mkusanyiko pindi itapokuyumkinia kufanya hivo. Unapopata mkusanyiko au ukasikia adhaana katika msikiti ulio karibu nawe basi ni lazima kwako kumuitikia muadhini na uhudhurie pamoja na mkusanyiko. Usiposikia adhaana na wala kusiwe na msikiti karibu nawe basi Sunnah ni wewe kuadhini na kukimu. Imethibiti kwamba Abu Sa´iyd (Radhiya Allaahu ´anh) alimwambia bwana mmoja: “Ukiwa kati ya mifugo wako au shambani mwako basi ipaze sauti yako kwa kuadhini. Hakika mimi nimemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Hakuna kinachosikia sauti ya muadhini – iwe mti, jiwe wala chochote chengine – isipokuwa kitamtolea ushuhuda siku ya Qiyaamah.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/351)
  • Imechapishwa: 19/09/2021