Kuadhibiwa mpaka kuuliwa kwa matendo ya uzinzi na kuwanajisi wanyama katika Biblia

10Sasa mwanamume anayefanya uzinzi na mke wa mwanamume mwingine ni mwanamume anayefanya uzinzi na mke wa mwenzake lazima auawe, mwanamume huyo mzinzi na vilevile mwanamke huyo mzinzi. 11Na mwanamume anayelala na mke wa baba yake ameufunua uchi wa baba yake.  Lazima wote wawili wauawe. Damu yao wenyewe iko juu yao. 12Na mwanamume akilala na binti-mkwe wake, lazima wote wawili wauawe. Wamevunja jambo la asili. Damu yao wenyewe iko juu yao. 13Na mwanamume akilala na mwanamume sawa na vile mtu anavyolala na mwanamke, wote wawili wamefanya jambo lenye kuchukiza. Lazima wauawe. Damu yao wenyewe iko juu yao. 14Na mwanamume akimchukua mwanamke pamoja na mama yake, ni mwenendo mpotovu.  Watamteketeza yeye na wao katika moto; ili mwenendo mpotovu usiendelee katikati yenu.

15Na mwanamume akimpa mnyama shahawa yake imtokayo, lazima auawe, nanyi mtamuua mnyama huyo. 16Na mwanamke akimkaribia mnyama yeyote ili kuungana naye, mtamuua mwanamke huyo na mnyama huyo. Lazima wauawe. Damu yao wenyewe iko juu yao.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Walawi 20:10
  • Imechapishwa: 12/01/2020