Swali: Mwanamke kutoka Uingereza anauliza kama inafaa kwake kuacha uso wazi mbele ya kaka yake mume? Isitoshe mama yangu hapendi mimi niivae lakini hata hivyo mimi naipenda sana. Unaninasihi nini?

Jibu: Nakunasihi kulazimiana na hukumu za Shari´ah na wala usimjali yeye wala mwengine yeyote. Hukumu ya Shari´ah inasema kufunika uso mbele ya wasiokuwa Mahram. Haijalishi kitu hata kama ni kaka yake mume.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 15/04/2021