Kuacha redio, simu au kompyuta yacheza na huku waingia chooni


Swali: Mimi nyumbani nina kifaa cha kurekodi ambacho kinasikika kwa mbali. Je, inajuzu kwangu kuingia chooni na huku kinacheza ima Qur-aan, muhadhara au kitu kingine au ni lazima nikizime?

Jibu: Hakuna ubaya juu ya hili. Inajuzu kwa mtu kuweka kifaa cha kurekodi nje ya mlango wa choo na huku anasikiliza. Kumesemekana juu ya babu wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, naye ni ´Abdus-Salaam, ya kwamba alikuwa akimuamrisha mtoto wake wa kiume kumsomea na yeye huku yuko chooni. Akifanya hivi kwa sababu ya kulinda wakati. Huenda haya ni katika mambo yenye kutokea kwa uchache. Kwa sababu sidhani kuwa kuna mwanachuoni anayefanya hivi siku zote. Lakini huenda anakuwa anataka kurejea masuala fulani na hivyo anafanya jambo hili. Pamoja na kuwa mimi naonelea kuwa inafaa. Lakini kuacha kufanya hivo ndio bora zaidi. Kwa nini? Kwa sababu ikiwa mtu atasikiliza Hadiyth yenye kumpendeza basi huenda akarefusha kukidhi haja na akakaa masaa na masaa. Kama inavyosemekana ya kwamba nchi za kikafiri pindi mtu anapotaka kusoma gazeti basi anaingia nalo chooni. Mnajua namna viti vyao vya choo vinavyokuwa ni hivi vya kizungu. Basi atakaa kwenye kiti hiki na huku yuko na gazeti. Si ajabu pia akawa na sigara.

Msikilizaji: Huweka kabati ndogo ya vitabu pia.

Ibn ´Uthaymiyn: Wanaweka kabati ya vitabu chooni? Tunamuomba Allaah afya:

إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا

“Wao si chochote isipokuwa ni kama wanyama, bali wao wamepotea zaidi njia.” (25:44)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/719
  • Imechapishwa: 09/11/2017