Swali: Masiku kadhaa ya nyuma kumetoka fatwa kutoka katika wizara ya mambo ya kutoa fatwa (دار الإفتاء) inayokataza mipasuko na migawanyiko. Baadhi wameijumlisha fatwa hiyo na kusema kwamba haijuzu kumraddi anayekwenda kinyume wala mzushi…

Jibu: Haya hayapo katika ubainifu. Ubainifu hausemi kuwa asiraddiwe anayekwenda kinyume, wala kusibainishwe haki kutokamana na batili. Huu ni uongo juu ya ubainifu. Ubainifu unawanasihi wanafunzi waache migogoro na mipasuko na kufanyiana uadui kati yao kwa sababu ya tofauti ndogondogo zinazotokea kati yao au kufahamiana vibaya. Badala yake wanatakiwa kunasihiana. Haya ndio malengo ya ubainifu. Kuifasiri juu ya matamanio yao wao ndio wenye kubeba jukumu hilo. Ubainifu uko wazi. Hakuna utatizi katika ubainifu huo. Wako wengi ambao wameyafasiri maneno ya Allaah juu ya matamanio yao. Wameyafasiri vile wanavotaka. Hiki si kitu kinachofanywa kwa ajili ya ubainifu peke yake. Watu wa batili hufuata batili zao na wanataka kitu kinachosapoti batili zao hata kama ni kuwasemea uongo watu, Qur-aan na wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 23/04/2021