Kuacha kusoma kwa sauti ya juu


Swali: Ni ipi hukumu ya kuacha kusoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu?

Jibu: Wanazuoni wanaona kwamba kusoma kwa sauti ya juu na kimyakimya ni miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa. Wamesema kuwa kusoma kwa sauti ya juu na kimyakimya ni miongoni mwa mambo yaliyopendekezwa ya swalah. Lakini haitakikani kwa mtu katika hali yoyote kukusudia kuacha kusoma kwa sauti ya juu katika swalah za kusoma kwa sauti ya juu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 19/06/2021