Swali: Ramadhaan iliyopita ilitokea nikala siku kadhaa pasi na udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Je, inatosha kwangu kulipa siku hizo peke yake? Kipi kinachonilazimu mbali na hayo? Mimi najutia hilo majuto makubwa na nimeazimia – Allaah akitaka – kutorudi katika mfano wa kitendo kama hicho?

Jibu: Kula mchana wa Ramadhaan pasi na udhuru ni kosa na jinai kubwa. Ni lazima kwa ambaye alifanya hivo atubu kwa Allaah tawbah ya kweli na ajutie yaliyotokea. Asirudi kufanya hivo katika mustakabali na ahifadhi swawm yake. Ukiongezea juu ya tawbah ni lazima alipe zile siku zilizompita. Ni lazima kwako ulipe siku hizi zilizokupita baada ya kutubu kwa Allaah. Pengine Allaah akakusamehe yaliyotangulia.

Swali: Je, analazimika kulisha chakula sambamba na kulipa?

Jibu: Ikiwa alifikiwa na Ramadhaan nyingine kabla ya kufunga bila ya udhuru basi ni lazima kwake kulisha chakula kwa kila siku moja iliyompita sambamba na kulipa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/415)
  • Imechapishwa: 22/03/2022