Kuacha kufunga Ramadhaan kwa sababu ya masomo

Swali: Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika ngazi ya sekondari. Mtihani mwingine utakuwa katika Ramadhaan. Kama unavyojua masiku ya mtihani mwanafunzi anakuwa anahitajia nguvu na kutoa juhudi zake kwa vile masiku ya mtihani ni yenye kufuatana mfululizo. Naona kuwa kufunga kunahitajia mapumziko na kulala. Je, inajuzu kula katika yale masiku ya mitihani kisha kuyalipa katika masiku mengine?

Jibu: Haijuzu kula kutokana na uliyoyasema. Bali imeharamishwa kufanya hivo. Kwa sababu mambo hayo hayaingii katika nyudhuru zinazomruhusu mtu kuacha kufunga katika Ramadhaan.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/240)
  • Imechapishwa: 10/06/2017