Swali: Wale ambao wanaabudu makaburi na wanawaomba msaada majini na wanafanya mambo mengine ya shirki yaliyo wazi. Mtu akiwaendea watu mfano ya hawa aanze kuwalingania katika ´hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah` au kwa msemo mwingine katika Tawhiyd au aende nao hatua kwa hatua mpaka hatimaye baada ya muda awafahamishe?

Jibu: Aanze kuwalingania Tawhiyd. Kwa sababu matendo yao hayatowanufaisha kitu isipokuwa baada ya Tawhiyd.

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa watu wanakimbia kwa kuanza kwa kitu kama hicho.

Jibu: Huu ni ujinga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alianza kwa Tawhiyd. Hakuanza kwa swalah, zakaah wala kutoa swadaqah. Bali alianza kuwalingania watamke shahaadah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 09/09/2019