Kuacha baadhi ya Sunnah kwa sababu ya kuleta umoja

Swali: Inajuzu kuacha baadhi ya Sunnah kwa kuchelea kutokea kwa fitina au kufarikiana kwa baadhi ya waislamu?

Jibu: Ni kama kwamba – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – anakusudia kuacha kunyanyua mikono miwili ndani ya swalah. Kwa sababu baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa kunyanyua mikono miwili ndani ya swalah wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam. Wanamkataza yule mwenye kunyanyua mikono yake wakati wa kwenda katika Rukuu´, kuinuka kutoka katika Rukuu´ na wakati wa kusimama kutoka katika Tashahhud ya kwanza. Je, bora ni kwenda kinyume na yale waliyomo kwa ajili ya kufuata Sunnah au bora ni kuacha kutendea kazi Sunnah kwa sababu ya kuziunganisha nyoyo zao? Maoni haya ya pili ndio bora. Lakini pamoja na hivyo asiache Sunnah moja kwa moja. Aitendee kazi nyumbani kwake na awafunze watu hawa kwamba haki ni kunyanyua mikono miwili. Kisha wakishapata utulivu wa maoni yake ndio wanyanyue mikono yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1499
  • Imechapishwa: 06/02/2020