Kosa linalofanywa na wanafunzi wengi

Muislamu akijifunza hukumu ya Kishari´ah kutoka kwa mwanachuoni anayetambulika na kisha baadaye akaulizwa hukumu hiyohiyo, haijuzu kwake kusema kuwa ni halali au ni haramu. Anachotakiwa ni yeye kusema kuwa amemsikia fulani amesema hivi na hivi. Watu wengi wa kawaida bali mpaka wanafunzi wanakosea katika jambo hili.

Pindi mmoja wao anapoulizwa juu ya suala fulani ambalo amelisikia kutoka kwa mwanachuoni, anamjibu kwa njia ambayo wale wasikilizaji wanadhania kuwa ni mwanachuoni. Pamoja na kuwa sio mwanachuoni. Bali amemsikia tu mwanachuoni akisema hivo. Ndio maana haitakiwi mwanafunzi kujiweka kimbelembele na kujionyesha kwa wengine kuwa ni mwanachuoni. Inamfanya kujifananisha kwa kitu ambacho hakupewa. Huenda hilo likamfanya kujikweza, akawadharau wengine na kuingiwa na kiburi kwa kitu ambacho bado hajafikia.

Kuna elimu aina mbili:

1- Elimu ambayo mtu amefikia. Elimu hii mtu anaweza kuitolea fatwa.

2- Eimu ambayo mtu ameipokea kutoka kwa mwengine. Hapa anatakiwa kunukuu.

Watu wawili hawa hawawezi kulinganishwa. Haya ndio nawanasihi kwayo ndugu zangu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (828)
  • Imechapishwa: 26/01/2019