Muislamu wa kawaida akijifunza hukumu ya Kishari´ah kutoka kwa mwanachuoni anayetambulika kisha baadaye akaulizwa na mwengine juu ya hukumu hiyohiyo, haijuzu kwake kusema kuwa ni halali au haramu. Hapa anatakiwa kusema kuwa amemsikia mwanachuoni fulani akisema kadhaa na kadhaa. Hili ni kosa linalofanywa na watu wengi wa kawaida mpaka na wanafunzi.

Pindi mmoja wao anapoulizwa juu ya suala fulani alilolisikia kutoka kwa mwanachuoni, anajibu kwa njia inayowafanya wasikilizaji kufikiria kuwa yeye pia ni mwanachuoni. Hata hivyo yeye sio mwanachuoni. Bali yeye amemsikia tu mwanachuoni akisema hivo. Kwa ajili hiyo mwanafunzi asijiingize na kujionyesha mbele ya wengine kwamba na yeye ni mwanachuoni.  Hivyo anakuwa ni mwenye kujifananisha kwa kitu ambacho sivyo alivyo. Pengine hata ikampelekea kujikwaza, kuwadharau wengine na akaingiwa na kiburi kwa kitu ambacho ukweli wa mambo hajakifikia.

Kuna elimu aina mbili:

1- Elimu yenye kutoka kwa mtu mwenyewe. Hii anaweza kuitolea fatwa.

2- Elimu aliyoipokea kutoka kwa mwengine. Hapa anatakiwa kumnukuu.

Wala watu wawili hawa hawawezi kulingana. Hichi ni kitu ambacho nawanasihi ndugu zangu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (828)
  • Imechapishwa: 26/09/2020