Swali: as-Suyuutwiy (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Itqaan fiy ´Uluum-il-Qur-aan” ya kwamba Jibriyl aliichukua Qur-aan kutoka katika Ubao uliohifadhiwa kisha akainakili. Je, haya ni sahihi?

Jibu: Ni kosa. Ni kosa la as-Suyuutwiy. Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) amemraddi kwenye kijitabu. Kuna kijitabu kimechapishwa pamoja na fataawaa za Shaykh Muhammad bin Ibraahiym. Amemraddi as-Suyuutwiy maneno yake haya ya kwamba Jibriyl aliichukua Qur-aan kutoka katika Ubao uliohifadhiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (58) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16539
  • Imechapishwa: 23/09/2017