Madhehebu ya Ashaa´irah wanaona kwamba imani ni kule mtu kusadikisha tu. Hawayaingizi matendo ya viungo. Wanasema kwamba japokuwa matendo yameitwa kuwa ni imani katika Hadiyth mbalimbali, hilo ni kwa njia ya majaaz na sio kihakika.

Ama madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba imani ni kusadikisha kwa moyo, kuzungumza kwa ulimi na matendo ya viungo. Kuna kundi la wanachuoni ambao wamewakufurisha wale wenye kuyaondosha matendo nje ya imani.

Ikishathibiti yale tuliyoyataja ya kwamba madhehebu ya Ashaa´irah wanamkanushia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) sifa Zake mbali na zile saba tulizotaja na wanaona kwamba Allaah hazungumzi kwa herufi na sauti, kwamba herufi za Qur-aan zimeumbwa, wanadai kwamba maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni maana moja na kwamba Qur-aan ndio hiyohiyo Tawraar na Injiyl. Lakini ikiabiriwa kwa kiarabu basi hiyo ni Qur-aan. Ikiabiriwa kwa kiebrania basi hiyo ni Tawraat. Ikiabiriwa kwa kisyria basi hiyo ni Injiyl. Hawathibitishi kuwa waumini watamuona Mola wao Peponi kwa macho yao.

Ukishayajua hayo basi utatambua kosa la wale waliowafanya Ashaa´irah eti ni katika Ahl-us-Sunnah. Hayo yamefanywa na Safaariyniy katika baadhi ya maneno yake. Huenda alifanya hivo kwa sababu ya kutaka kuwapaka mafuta kwa sababu wao hii leo ndio watu wengi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan Abaa Butwayn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Rasaa-il wal-Masaa-il an-Najdiyyah (02/178)
  • Imechapishwa: 19/03/2019