Swali: Kuandika “an-Naas” na “al-Falaq” na Aayah ya “al-Kursiy” katika karatasi kisha mtu akaweka ndani ya kikombe cha maji kwa ajili ya kumtabana mtu ambaye amepatwa na kijicho. Je, njia hii ni inakubalika katika Shari´ah?

Jibu: Haya ni matabano. Maimamu, akiwemo Imaam Ahmad na Ibn-ul-Qayyim[1], wamesema kuwa hakuna neno kuziandika Aayah na du´aa kwenye sahani au kwenye karatasi kisha mtu akamwagilia maji masafi na mgonjwa akayanywa. Hii ni moja ya matabano yanayofaa.

[1] Zaad-ul-Ma´aad (04/170).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 40
  • Imechapishwa: 23/05/2021