Kodi kwanza, ununue baadaye

Swali: Kampuni inauza magari kisha baadaye wanayakodisha kwa kipindi cha miaka mitatu kwa bei kadhaa. Je, inajuzu?

Jibu: Huku ni kukusanya kati ya kuuza na kukodisha na haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza biashara mbili katika biashara moja. Kwa msemo mwingine ni kwamba wanakushurutisha ukodi ili baadaye waje kukuuzia nayo. Ni kitendo cha haramu na hakijuzu. Lakini wakikuuzia nayo bila kukushurutisha kuikodi ambapo baadaye wakataka kuikodisha kwake, hapana neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 05/02/2022