Kiwango cha Zakaat-ul-Fitwr kwa mujibu wa Ibn Baaz


Swali: Zakaah baada ya Ramadhaan kunatolewa kiwango gani?

Jibu: Nadhani kwamba muulizaji anamaanisha Zakaat-ul-Fitwr inayotolewa baada ya Ramadhaan. Ni wajibu kutoa pishi moja katika chakula kinacholiwa katika mji. Inaweza kuwa mchele, shayiri, tende au chakula kingine kinacholiwa katika mji. Anatakiwa kutoa mvulana, msichana, muungwana, mmilikiwa, mdogo na mkubwa ambao ni waislamu, kama zilivyosihi kuhusu hilo Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni wajibu kuitoa kabla watu hawajatoka kuswali ´Iyd. Ni sawa vilevile kuitoa siku moja au siku mbili kabla ya ´Iyd. Kiwango chake – tukizungumzia kg – ni karibu 3 kg. Haijuzu kutoa pesa. Bali ni wajibu kutoa chakula kinacholiwa katika mji, kama tulivyokwishatangulia kusema.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/203)
  • Imechapishwa: 12/06/2018