Kiwango cha kutenzwa nguvu kinachompelekea mtu kukufuru

Swali: Ni kipi kiwango cha kutenzwa nguvu ambacho yule mwenye kutumbukia ndani yake hazingatiwi kuwa ni mwenye kuritadi? Je, kuna aina za kulazimishwa?

Jibu: Kutenzwa nguvu kunatofautiana kutegemea hali. Kutenzwa nguvu kunaweza kuwa katika jambo na kusiwe katika jambo jengine. Kutenzwa nguvu kutegemea na hali yake. Lakini hata hivyo kutenzwa nguvu ambako mtu anapewa udhuru ni kule ambako mtu hawezi kujinasua, kusalimika na kuuawa, kupigwa au kutishwa isipokuwa mpaka atamke yale anayotakwa. Kwa mfano kutamka neno la kufuru. Ikiwa hawezi kujinasua na dhuluma za dhalimu isipokuwa mpaka atamke, basi afanye hivo. Kwa sharti moyo wake ubaki umetua juu ya imani. Amesema (Ta´ala):

إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ

”… isipokuwa yule aliyelazimishwa na huku moyo wake ukawa umetua juu ya imani.” (an-Nahl 16:106)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 33
  • Imechapishwa: 22/11/2019