2682 – Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ee ´Amr! Hakika Allaah (´Azza wa Jall) amekimairi kila kitu umbile lake.” Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akapiga kwenye goti la ´Amr kwa vidole vyake vinne vya mkono wa kulia na akasema: “Ee ´Amr! Hapa ndipo pahali pa kikoi.” Halafu akakinyanyua kisha akapiga kwa vidole vyake vinne chini ya sehemu vilivyokuwa mara ya mwanzo. Kisha akasema: “Ee ´Amr! Hapa ndipo pahali pa kikoi.” Halafu akakinyanyua kisha akapiga kwa vidole vyake vinne chini ya sehemu vilivyokuwa mara ya pili. Akasema: “Ee ´Amr! Hapa ndipo pahali pa kikoi.”

Ameipokea Ahmad (4/200): al-Waliyd bin Muslim ametuhadithia: al-Waliyd bin Sulaymaan ametuhadithia kwamba al-Qaasim bin ´Abdir-Rahmaan amewahadithia, kutoka kwa ´Amr bin Fulaan al-Answaariy.

Cheni ya wapokezi ni nzuri na wapokezi wake ni waaminifu.

Miongoni mwa mambo ya kushangaza ni kwamba baadhi ya watu ambao wako na kitu katika elimu ya kiislamu wanajaribu kujuzisha kurefusha nguo chini ya kongo mbili za miguu kwa sababu ya Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Yule ambaye ataburuza nguo yake kwa kiburi basi Allaah hatomwangalia siku ya Qiyaamah.” Ndipo Abu Bakr akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika upande mmoja wa kikoi changu unashuka licha ya kuwa napambana nacho.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Wewe si miongoni mwa wale wanaoburuza kwa kiburi.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Ahmad. Katika upokezi mwingine imekuja:

“Baadhi ya nyakati kinashuka.”

Katika Hadiyth kuna dalili ya wazi kwamba Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) hakuwa akirefusha nguo yake; bali kilikuwa kinamshuka pasi na yeye kukusudia. Pamoja na hivyo anapambana kukipandisha. Haafidhw Ibn Hajar amesema:

“Ni kama kwamba ufungaji wake ulikuwa unafunguka pindi anapotikisika kwa kutembea au kwa kufanya kitu kingine. Yalikuwa yakimtokea pasi na yeye kukusudia kwa sababu alikuwa akipambana kisimshuke chini. Kwa sababu kila kinapomshuka basi anakifunga vizuri.”[1]

Je, inafaa kutumia hoja kwa kisa hiki? Tofauti iko wazi kabisa kati ya Abu Bakr ambaye yalikuwa yakimtokea kukusudia na mtu ambaye daima anavaa nguo yake chini ya kongo mbili za miguu kwa makusudi. Tunamuomba Allaah ulinzi kutokamana na matamanio.

[1] Fath-ul-Baariy (10/217).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadîth as-Swahiyhah (6/1/410)
  • Imechapishwa: 26/08/2020