Kiungo hakikupatwa na maji kabla au baada ya swalah

Swali: Muislamu akibainikiwa baada ya kutawadha kwamba kuna sehemu ndogo kwenye kiungo haikupatwa na maji ikiwa ni kabla hajaswali au baada ya swalah?

Jibu: Ikiwa ni baada ya swalah basi atawadhe tena na airudi swalah yake. Ama ikiwa ni kabla ya swalah, ikiwa wakati ni mfinyu na hatowahi kutawadha [kikamilifu], basi aoshe sehemu hiyo kisha akamilishe wudhuu´ wake. Kwa mfano ameona sehemu hiyo ndogo ni mkononi na wakati wa swalah umekaribia, basi aoshe sehemu hiyo kisha apanguse kichwa chake na aoshe miguu yake. Mfano mwingine sehemu hiyo ikiwa ni mguuni basi aoshe mguu wake. Lakini wakati ukiwa mpana basi arudi kutawadha upya.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 01/05/2018