Kitu cha kuchezea cha wanaume


al-Mardaawiy amesema:

“Jua kuwa wanawake ni kitu chetu cha kuchezea. Kwa hiyo, angalia vyema iwezekanavyo.”

Wanawake ni kitu cha kuchezea ambacho mwanaume hucheza nacho. Kwa hiyo, unatakiwa uangalie uchague kitu cha kuchezea kilicho na heshima nzuri na dini. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kasema:

“Dunia ni starehe na bora ya starehe ni kuwa na mke mwema. Wakati anapomtazama anamfurahisha, na wakati mume yuko mbali nae, anamhifadhia heshima yake na mali yake.” (Muslim (1467))

Allaah (‘Azza wa Jall) amesema:

فالصالحات قانتات حافظات للغيب بما حفظ الله

“Basi wanawake wema watiifu, wenye kuhifadhi hata wanapokuwa hawapo kwa aliyoyahifadhi Allaah.” (04:43)

Wanawake bora ni wale walio na uinje na undani mzuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ittihaaf-ut-Twullaab, uk. 872-873
  • Imechapishwa: 22/09/2020