Kitabu “Tanbiyh-ul-Ghaalifiyn” kina Hadiyth nyingi zilizotungwa


Swali: Unasemaje juu ya vitabu vya kidini vinavyotoka nje ya Saudi Arabia ikiwa ni pamoja na kitabu “Tanbiyh-ul-Ghaalifiyn”?

Jibu: Muumini anatakiwa kutahadhari kila kitabu ambacho ndani yake kuna mambo yenye kuidhuru dini na kuna ulinganizi katika mambo ya ufisadi. Ni lazima kutahadhari kila kitabu, sahifa na gazeti linaloeneza maharibifu, propaganda za batili au fikira za kuangamiza. Vilevile ni lazima kutahadhari gazeti la picha za nyuchi.

Kuhusu “Tanbiyh-ul-Ghaalifiyn” viko viwili. Kimoja ni cha Ibn-un-Nahaas ambacho ni kitabu kizuri na chenye faida. Kitabu cha pili ni cha al-Layth as-Sarmaqandiy ambacho ndani yake kuna Hadiyth ambazo zimetungwa na Hadiyth dhaifu ambazo hazitakiwi kutegemewa. Hiki cha pili ni kitabu cha al-Layth as-Sarmaqandiy. Kuhusu hicho cha kwanza cha Nahaas ni kitabu kizuri ambacho ndani yake mna nyasia na maelekezo mazuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4429/%D9%85%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%A7%D9%8A-%D9%81%D9%8A-%D9%83%D8%AA%D8%A7%D8%A8-%D8%AA%D9%86%D8%A8%D9%8A%D9%87-%D8%A7%D9%84%D8%BA%D8%A7%D9%81%D9%84%D9%8A%D9%86
  • Imechapishwa: 26/09/2020