Kitabu Kilichojaa Takfiyr


Kuhusiana na Qutbiyyuun waliingia katika Takfiyr moja kwa moja. Soma vitabu vya al-Ikhwaan al-Muslimuun – wadanganyifu wa waislamu – na mtazama kama hamtoona mielekeo mingine isiyokuwa hii miwili.

Katika kipindi hichi cha mwisho Takfiyr imezidi kudhihiri zaidi na zaidi. Ni madhehebu ya Sayyid Qutwub. Hakuna kwengine ambapo yamekita madhehebu haya kama Saudi Arabia. Inasikitisha. Wanatumia fursa ya mapenzi ya watu wa nchi ya kupenda Tawhiyd na kutahadharisha shirki, wakapenyeza Tawhiyd-ul-Haakimiyyah na Shirk-ul-Haakimiyyah na wakafanya kuwa ni Tawhiyd ya aina ya kipekee. Kwa hivyo wakawa kila wakati wanazungumzia Tawhiyd peke yake, lakini njama zao ni kuwakufurisha waislamu.

Ninaapa kwa Allaah ya kwamba takriban miaka arobaini iliyopita nimesikia kwa masikio yangu wanavyosema kuwa kitabu “Ma´aalim fiyt-Twariyq”[1] ni ufupisho wa kitabu cha Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab “Kitaab-ut-Tawhiyd”. Kitabu chote kimejaa Takfiyr. Kitabu hichi mimi nakiita “Ma´aalim fiy Twariyq-it-Takfiyr”. Nakala yangu ya kwanza yacho iligawiwa na wizara ya Kiislamu. Kina stempu ya kijani. Mwenye kuchukia achukie. Ninawapa udhuru. Hawakutambua vitabu hivi. Hawakuvisoma. Wanachuoni wetu wenyewe walisema hivi. Waliokuwa chini wakapata vitabu hivi na wakawa ni wenye kuwafanyia ghushi ummah wa Kiislamu. Wanaharakati wakaanza kufanya kazi sehemu hizi, wakanunua vitabu hivi na kuvitawanya.

Ninachotaka kusema ni kwamba pote hili al-Ikhwaan al-Muslimuun ndio msingi wa mapote mengine yote haya, na al-Qaa´idah ndio msingi wa mapote mengine yote mapya kama ISIS, an-Nusrah na majina mengine yote wanavyoitwa.

——–
(1) Cha Sayyid Qutwub.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.miraath.net/fatwah/12009
  • Imechapishwa: 07/02/2017