Swali 32: Je, maneno haya ni sahihi kwamba kiongozi ni yule ambaye waislamu wote wamekusanyika juu yake kuanzia mashariki mpaka magharibi?

Jibu: Haya ni maneno ya Khawaarij. Imamu ni yule aliyeteuliwa na Ahl-ul-Hall wal-´Aqd katika waislamu. Ni lazima kwa waliobaki kumtii. Si lazima eti watu wote wampe kiapo cha usikivu na utiifu kuanzia magharibi mpaka magharibi, wanaume kwa wanawake. Huu sio mfumo wa Uislamu katika kuteua uongozi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 142
  • Imechapishwa: 28/09/2019