Swali: Je, ni kweli kwamba Ibn-ul-Jawziy ndiye ambaye kaandika kitabu hichi – Daf´ Shubah-it-Tasbiyh – pamoja na kuzingatia ya kwamba alikuwa Hanbaliy?

al-Albaaniy: Ndio, ni kweli kwamba alikuwa Hanbaliy, lakini unaamini kuwa kila Hanbaliy alikuwa amekingwa na makosa?

Swali: Hapana, sivo hivyo. Lakini mtu huyu alikuwa na nafasi kubwa katika kujeruhi na kusifu.

al-Albaaniy: Ndio, katika kujeruhi na kusifu, lakini hujui kuwa vilevile kuna Suufiyyah na wanachuoni katika kujeruhi na kusifu na Hadiyth?

Muulizaji: Ndio, bila shaka.

al-Albaaniy: Kwa hiyo ni hali kadhalika. Hujui kuwa Ibn-ul-Jawziy alisema kuwa Allaah (´Azza wa Jall) hayuko ndani ya ulimwengu wala nje yake?

Muulizaji:  Haya ni maoni ya Ashaa´irah?

al-Albaaniy: Ni maoni ya Ibn-ul-Jawziy.

Muulizaji:  Ndio, ni maoni ya Ibn-ul-Jawziy, lakini ni nani aliyesema kabla yake?

al-Albaaniy: Hayo yanahusiana na nini? Mimi nimekuuliza kama unajua kwamba Ibn-ul-Jawziy amesema kuwa hayuko ndani ya ulimwengu wala nje yake?

Muulizaji: Hapana, sijayasoma hayo. Hivi ndo napata kuyajua.

al-Albaaniy: Soma kitabu hicho utayapata. Huyo ndiye kiongozi wa khabithi huyu as-Saqqaaf.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=zOo_eandnv4&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 15/04/2018