Kiongozi Anatekeleza Shari´ah Hatua Kwa Hatua


Swali: Mtawala asiyeweza kubadili kanuni za watu zote kwa mara moja anaweza kulinganishwa na an-Najaashiy?

Jibu: Ndio. Ni kama mtawala ambaye anamuamini Allaah na Mtume Wake lakini hawezi kutekeleza hukumu ya Allaah kwa sababu wananchi zake makafiri wanaonelea kinyume. Atatekeleza kile anachokiweza:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid%207%20-%20... Toleo la: 22.05.2015
  • Imechapishwa: 11/02/2017