Kinywaji cha shayiri kilicho na alcohol kidogo


Swali: Ni ipi hukumu ya kunywa kinywaji cha shayiri ikiwa kina asilimiando ndogo kama mbili kwa mia ya alcohol?

Jibu: Mimi sijui kitu kuhusu kinywaji hicho. Lakini ikiwa kina asilimia kubwa ya alcohol ni haramu. Ama ikiwa kuna kitu kidogo ambacho hakionekani hakizingatiwi. Lakini hata hivyo ni jambo linahitajia kuangaliwa vizuri. Mtu huwezi kuhukumu kitu kabla ya kukiona. Mimi sijui kitu juu ya kinywaji hicho cha shayiri. Ikiwa hakina nyenzo zenye kulewesha hakina neno. Ama ikiwa kinywaji hicho kinapotengenezwa kinakuwa kingi na ndani yake kuna kitu kidogo, inaweza kusamehewa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 01/03/2018