Kinachozingatiwa katika kupangusa juu ya soksi ni ile hali ya mwisho kwa mtazamo wa Ibn ´Uthaymiyn

Swali: Nataka unipe mfano kuhusu kufuta juu ya khofu kwa mtu ambaye ni msafiri akipangusa juu ya khofu kisha akawa mkazi au mkazi akifuta kisha akasafiri. Ni ipi hukumu kwa sababu utatizi umekuwa mwingi.

Jibu: Kuhusu aliyepangusa kisha akasafiri basi atakamilisha kufuta kama msafiri. Kwa mfano mtu amefuta kwenye khofu siku nzima kisha na kabla ya kumalizika ule muda wa kupangusa akasafiri basi katika hali hii amebaki na siku mbili ambazo anatakiwa kupangusa. Ama kuhusu ambaye amepangusa akiwa ni msafiri kisha akawa mkazi, basi atakamilisha kupangusa kama mkazi. Kujengea juu ya hili akifika katika mji wake na kumeshampitia mchana na usiku wake, katika hali hii ni wajibu kwake kuzivua na atawadhe wudhuu´ kamilifu. Kwa hivyo kinachozingatiwa ni ile hali yake ya mwisho. Lakini hata hivyo akianza kupangusa hali ya kuwa ni mkazi na muda wa kufuta ukawa umeisha, basi katika hali hii inatambulika kuwa ni lazima azivue ndio azivae.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/732
  • Imechapishwa: 25/11/2017