Kinachozingatiwa katika kupangusa juu ya soksi ni ile hali ya mwisho kwa mtazamo wa Ibn ´Uthaymiyn II


Swali: Mtu akianza kupangusa kwenye soksi hali ya kuwa ni mkazi kisha akasafiri atatimiza kupangusa akiwa ni msafiri au mkazi?

Jibu: Msafiri. Haya ndio maoni yenye nguvu.

Swali: Mtu akianza kupangusa kwenye soksi hali ya kuwa ni msafiri kisha akarudi katika mji wake atatimiza kupangusa akiwa ni mkazi au msafiri?

Jibu: Atatimiza kupangusa hali ya kuwa ni mkazi. Muda ukiisha ni lazima kwake kuosha miguu yake.

Swali: Inajuzu kwa mtu ambaye anapangusa juu ya soksi kumwongoza katika swalah asiyepangusa?

Jibu: Ndio, inajuzu. Hili ni kama inavyojuzu kwa imamu ambaye amefanya Tayammum kumwongoza ambaye anaswali kwa wudhuu´.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (23)
  • Imechapishwa: 02/01/2019