Kinachofanywa swalah ya ´iyd ikiangukia ijumaa

Swali: Kufanywe nini swalah ya ´iyd ikiangukia siku ya ijumaa?

Jibu: Cha kufanywa ni kwamba waislamu wamepata sikukuu mbili; sikukuu ya wiki na sikukuu ya Ramadhaan. Yule ambaye amehudhuria swalah ya ´iyd hana ulazima wa kuhudhuria swalah ya ijumaa. Lakini hata hivyo anatakiwa kuiswali Dhuhr. Ama kuhusu imamu ni lazima kwake kuziswali zote. Misikiti mingine wasisimamishe Dhuhr. Tunachomaanisha ni kwamba hatuwaambii hiyo misikiti mingine waadhini na waswali Dhuhr, lakini tunachowaambia ni kwamba wahudhurie katika ule msikiti mkubwa. Yule ambaye hakuhudhuria ilihali amehudhuria na imamu swalah ya ´iyd, basi aiswali nyumbani kwake, shambani kwake au kwenginepo. Muhimu ni kwamba ile misikiti inayoswali swalah ya ijumaa isimamishe swalah siku hii iliokutana na ´iyd. Yule mwenye kuhudhuria ndio bora zaidi. Asiyehudhuria hapati dhambi ikiwa alihudhuria swalah ya ´iyd. Lakini kwa yule ambaye hatohudhuria aswali Dhuhr. Kwa sabbau ni faradhi ya wakati ambayo ni lazima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1645
  • Imechapishwa: 02/04/2020