Swali: Nina duka ambalo linashona ´Abaa´ah na naambatanisha pamoja na swali langu miundo nne ya ´Abaa´ah za kifaransa au za kimaroko ambazo zinapendwa sana na wanawake wengi na khaswakhaswa wasichana wanaoenda masomoni…

Jibu: Hapana shaka kwamba mwanamke kila ambavyo atajisitiri zaidi ndivo anavyokuwa karibu zaidi na Sunnah, heshima na hayaa ambayo ni sifa moja wapo ya muumini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hayaa ni katika imani.”

Mavazi na ´Abaa´ah hizi zilizo na vitambara vya viunganishio vya mikono, tayari vina makatazo kabla ya kuwa na mapambo. Makatazo yake ni kwamba vinaonyesha mwili wa mwanamke. Kwa sababu ´Abaa´ah hii ataiweka juu ya mabega yake, aonyeshe kichwa chake na shingo yake. Sijui atajisitiri kichwa chake kwa kitu gani. Pengine ni shungi na Niqaab yenye mapambo.

Kwa ajili hiyo nawanasihi wasichana wetu, watoto zetu wa kike, ndugu zetu na shangazi zetu wajiepushe na ´Abaa´ah hizi.

Kuhusu wale wanaozileta nawanasihi pia kutozileta na badala yake walete ´Abaa´ah zile za zamani zilizokuwa na sitara kamilifu na wajiepushe na mionekano ya fitina ambayo ndio bidhaa zao. Wakiachana na hizo ´Abaa´ah ambazo wametutajia punde tu kwa ajili ya Allaah, basi Allaah atawapa badala yake kilicho bora kuliko hizo kwa kuwapa baraka, kutokuwa, tamaa na uroho. Kwa sababu hakuna mtu yeyote anayechuma mali kwa njia ya haramu isipokuwa Allaah huweka moyoni mwake uroho na kuipupia dunia na mwishowe anakuwa kama mtu ambaye anakula bila ya kushiba.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (53) http://binothaimeen.net/content/1205
  • Imechapishwa: 21/08/2019