Kimsingi ni kwamba vichinjwa vya mayahudi na manaswara ni halali kwa waislamu


Swali: Kuku zinazotoka nchi za nje zinaingia katika mambo yenye kutatiza?

Jibu: Msingi ni kwamba vichinjwa vya Ahl-ul-Kitaab ni halali kwetu. Amesema (Ta´ala):

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ

“Chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu.” (05:05)

Ahl-ul-Kitaab ni mayahudi na manaswara.

Kuhusiana na vichinjwa vinavyotoka katika miji ya kikomunisti si halali. Wao si Ahl-ul-Kitaab. Mtu akitatizika na asijue kama wanachinja au hawachinji kwa njia ya Kiislamu, basi vinaingia katika mambo yenye kutatiza. Katika hali hiyo itatakiwa kujiepusha navyo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kiache kile chenye kukutia mashaka na kiendee kile kisichokutia mashaka.”

Himdi zote anastahiki Allaah kuku leo zimeenea katika nchi za Kiislamu. Mtu anatakiwa kuisalimisha dini yake na wala asije vichinjwa vyenye kutoka nje ikiwa vina mashaka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 05/02/2018