Kila swawm ya wajibu inatiwa nia usiku

Swali: Je, swawm ya kafara ya yamini ni lazima mtu kutia nia wakati wa usiku kabla ya kuanza kufunga?

Jibu: Ndio. Kila swawm ya wajibu; sawa ikiwa ni ya kafara, nadhiri au swawm ya Ramadhaan, ni lazima mtu atie nia wakati wa usiku. Ama kuhusu swawm ya Sunnah, ni sahihi mtu akatia nia wakati wa mchana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (61) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13585
  • Imechapishwa: 16/11/2014