Swali: Je, Jamaa´at-ut-Tabliyh na al-Ikhwaan al-Muslimuun ni katika mapote potevu?

Jibu: Kila mwenye kwenda kinyume na yale aliyomo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake, anaingia katika mapote potevu. Lakini upotevu wake unaweza kuwa upotevu ulio wazi kabisa na upotevu wake unaweza kuwa chini ya hapo. Wanatofautiana. Vinginevyo kila mwenye kwenda kinyume na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale aliyomo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake kwenye ´Aqiydah, anaingia katika mapote potevu. Upotevu wake unaweza kuwa wa unisba kwa kiasi cha upotevu watakaokuwa nao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_03.mp3
  • Imechapishwa: 02/07/2018